TPBA YAFANYA KIKAO MAALUM NA MHE.JOHARI
24 Sep, 2026
TPBA YAFANYA KIKAO MAALUM NA MHE.JOHARI

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.Hamza S.Johari amekielekeza chama cha (TPBA) kuendelea na utekelezaji wa mpango mkakati wa chama na kuhakikisha wanasimamia vyema chama chao na kukifanya kuwa miongoni mwa vyama bora vya kitaaluma,chama chenye kuzingatia weledi na maadili ya taaluma ya mawakili.

Mhe. Hamza S. Johari Mwanasheria Mkuu wa Serikali

 Mhe.Johari amesisitiza kuwa ni lazima mawakili wa serikali wachukue nafasi ya kuelimisha jamii kuhusu masuala ya post truth ( kipindi cha baada ya ukweli) zama hizi watu wanapenda taarifa za uongo na uzushi kuliko taarifa za ukweli.

 

Vilevile Mhe.Johari amesema Taarifa za uongo na uzushi zinaenea kwa kasi zaidi kuliko taarifa halisi za ukweli hivyo ni vzuri mawakili wa serikali kuweka mikakati ya namna ya kukabiliana na dhana hiyo.

 

Aidha amesisitiza kwamba chama lazima kiwe na manufaa Makubwa kwa wananchi.

 

kwa upande wake Rais wa Chama cha mawakili wa Serikali Tanzania (TPBA) Mhe.Bonaventure Pardon Mwambaja alieleza Kuwa wameyapokea maelekezo hayo ya mwanasheria Mkuu wa Serikali na wataenda  kujipanga na kuweka mikakati ya utekelezaji wa yote ambayo Mhe.Johari amewaelekeza.

 

Sambamba na hayo Mhe. Mwambaja amesema kuwa wanakuja na mpango wa uelimishaji umma kuhusiana na "post-truth" na namna ambavyo mambo haya yanaleta athari kubwa kwenye Taifa la Tanzania.

Mhe.Bonaventure P. Mwambaja Rais TPBA

"Tunaendelea kutekeleza maelekezo ya Mhe. Rais Dr. Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,maelekezo ambayo Mhe.Johari ameyasisitiza tena kuwafikia wananchi wanyonge na kuendelea kutoa huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi kila sehemu" amesema Mhe.Mwambaja.

Settings