TANGAZO LA KUONGEZA MUDA WA KUCHUKUA NA KURUDISHA FOMU KWA WAGOMBEA WA NAFASI MBALIMBALI KATIKA CHAMA CHA MAWAKILI WA SERIKALI
----------------------
Rejea Tangazo la Uchaguzi wa Viongozi Chama cha Mawakili wa Serikali (Public Bar Association) lililotolewa tarehe 16 Februari 2024, na kutoa ratiba ya Uchaguzi. Hata hivyo, Baadhi ya nafasi za Uongozi zimekosa wagombea.
Hivyo, Kamati ya Uchaguzi, imeamua kutoa muda wa nyongeza wa siku tatu (3) kwa ajili ya kutoa nafasi nyingine ya kuchukua na kurudisha Fomu. Kwa Tangazo hili, Mawakili wote wa Serikali mnajulishwa kuwa muda wa kuchukua na kurudisha fomu za kugombea nafasi za Uongozi wa Chama umeongezwa kuanzia tarehe 01 Machi, 2024 hadi 03 Machi, 2024.
Kufuatia mabadiliko hayo, Ratiba ya Uchaguzi itakuwa kama ifuatavyo:-
- 01/03/2024 – 03/03/2024 – kuchukua na kurudisha Fomu
- 04/03/2024 – 10/03/2024 – Vikao vya kuchuja Wagombea
- 11/03/2024 – Majina ya Wagombea Waliopitishwa Kutangazwa; na
- 12/03/2024 – 21/03/2024 – Kampeni kwa Wagombea Waliopitishwa
- 22/03/2024 – Siku ya Uchaguzi
Kwa mawasiliano tafadhali wasiliana na:
Bi. Juliana Changarawe: +255 788 473 707
Bw. Kadete Mihayo: +255 716 893 585
Bi. Jennifer Kaaya: +255 715 778 999
Bw: Reward Mriya: +255 758 906 875
Bw: Ludovick Ringia: +255 714 560 460
SIA MREMA
KATIBU
29/02/2024